Leviticus 8:1-6

Kuwekwa Wakfu Kwa Haruni Na Wanawe

(Kutoka 29:1-37)

1 Bwana akamwambia Musa, 2 a“Waletee Haruni na wanawe mavazi yao, mafuta ya upako, fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo dume wawili na kikapu chenye mikate iliyotengenezwa bila chachu. 3 bKisha kusanya mkutano wote kwenye ingilio la Hema la Kukutania.” 4Musa akafanya kama Bwana alivyomwagiza, na mkutano ukakusanyika kwenye ingilio la Hema la Kukutania.

5Musa akaliambia kusanyiko, “Hili ndilo Bwana ameagiza lifanyike.” 6 cKisha Musa akamleta Haruni na wanawe mbele, akawaosha kwa maji.
Copyright information for SwhKC